

Shauri la Madai Namba 23/2016 THE REGISTERED TRUSTEES OF THE CIVIC UNITED FRONT (CUF-CHAMA CHA WANANCHI) dhidi ya Msajili wa vyama vya siasa nchini (THE REGISTRAR OF THE POLITICAL PARTIES)-1,
Mwanasheria Mkuu wa Serikali (THE HONOURABLE ATTORNEY GENERAL)-2,
Prof Ibrahim Haruna Lipumba-3,
Magdalena Sakaya-4,
Maftaha Nachuma-5
Abdul Kambaya-6,
Masudi Omari Mhina-7,
Thomas Malima-8,
Kapasha H. Kapasha-9,
Musa Haji Kombo-10,
Habibu Mnyaa-11,
Na Haroub Shamis-12.
Leo limefikishwa mbele ya Jaji Kihiyo na kupangiwa ratiba ya uwasilishaji wa majibu kama ifuatavyo; Mpaka tarehe 17/11/2016 wadai wote wawe wameshawasilisha (ku-file) majibu yao (Counter Affidavit), na tarehe 23/11/2016 CUF iwe imeshawasilisha (ku-file) majibu kama itapenda kufanya hivyo (Reply to Counter Affidavit) Tarehe 24/11/2016 itatajwa kwa mara ya pili na kupangwa tarehe ya kusikilizwa.
CUF imewakilishwa na Mawakili wasomi Mhe. Daimu Halfani na Mhe. Nassor Juma, wakati Msajili wa vyama vya siasa aliwakilishwa na Sisty Nyahoza, Mwanasheria Mkuu wa serikali aliwakilishwa na wakili wake. Aidha, Prof Ibrahimu Lipumba na wenzake wamewakilishwa na Albert Msando ambaye ni wakili kutoka chama cha ACT-Wazalendo, pamoja na Mashaka Ngole. Wadaiwa wote walihudhuria mahakamani isipokuwa wadaiwa namba 4, 5, na 9, hapo juu. Wadaiwa wote wamepata Summons na wadaiwa 12 wamekubaliana kufanya majibu ya pamoja (Joint Reply).
Mawakili wetu wametuhakikishia kuwa wamejipanga vizuri na kututaka tuendelee kuwa na subra wakati wakiendelea kuandaa HOJA NGANGARI dhidi ya wadaiwa wote. Tunawapongeza wanachama wetu wote na walinzi wa chama NGANGRI kwa kujitokeza kwa wingi na kuwalinda vyema viongozi wetu wote dhidi ya MUNGIKI waliokusudia kutaka kuanzisha uhuni wao mahakamani. Tukutane tena mahakamani tarehe 24 NOVEMBER, 2016 saa 3 Asubuhi.
CUF TAASISI IMARA, CUF NGANGARI,
HAKI SAWA KWA WOTE
Maharagande
KNMHUMU
0 MAONI YAKO:
Post a Comment