Esma PlatnumzDada wa msanii Diamond
platnuz Esma Platnumz amesema hakuwahi kumtabiria wala kutegemea kuwa
kaka yake Diamond angekuja kuwa mtu maarufu kimataifa japo alikuwa
akionesha kupenda muziki tangu akiwa mdogo.
Hata
hivyo Esma amesema maswala yanayoandikwa kwenye magazeti kuhusiana na
Baba yake siyo ya kweli kwa kuwa yeye anamfahamu baba yake mzazi na mtu
aliyejitokeza kwenye magazeti siyo baba yake na hamfaham kabisa.
Pia Esma hakusita kuongelea taarifa zilizozagaa kwamba mama Daimond
hana mahusiano mazuri na wifi yao Zari na kusema hawana tatizo lolote na
wifi yao na hakuna mzazi asiye furahia wajukuu hivyo watu wanayoyaona
katika magazeti siyo ya kweli na wasiyatilie mkazo, huku akimalizia kwa
kusema kuwa anampenda mume wake Petit Man.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment