Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. William Lukuvi amewataka wananchi kutoa taarifa za raia wa kigeni wanaomiliki ardhi nchini kinyume cha sheria
Amesema
taarifa hizo zitaisaidia serikali kuzitwaa ardhi hizo kwa kuwa raia wa
kigeni hawaruhusiwi kumiliki ardhi nchini na kufanya hivyo ni kukiuka
sheria.
Akitoa hotuba kwenye mkutano Mkuu wa Mwaka wa Chama cha Wapima Ardhi
Tanzania (IST), Mhe. William Lukuvi amesema anayeruhusiwa kumiliki ardhi
nchini ni raia wa Tanzania pekee na kuongeza kwamba kwa watanzania
waishio nje ya nchi na kuukana uraia wao nao hawataruhusiwa kumiliki
ardhi bali watapewa ardhi kama ilivyo kwa wawekezaji kutoka mataifa
mengine.
“Mtu akishaukana uraia wa Tanzania hana haki tena kama raia wa
Tanzania, hivyo atamiliki ardhi kama mwekezaji na siyo raia, ardhi
itabaki kuwa ya Watanzania tu, tutawasaka wale wote ambao wanamiliki
ardhi kinyume na sheria za nchi,” amesema Mh. Lukuvi.
Aidha, Mhe Lukuvi amewataka wapima ardhi Tanzania kuhakikisha
wanatimiza lengo la serikali la kupika na kutoa hati 400,000 ifikapo
mwezi Juni mwaka 2017 pamoja na kutenga maeneo ya wafugaji kila wapimapo
ardhi.
Wadau hao wa upimaji ardhi wamesema, watahakikisha wanatimiza lengo
la serikali la kupima na kutoa hati 400,000 ifikapo Mwezi Juni 2017 kwa
kutumia vifaa vya kisasa sambamba na kuwekeza hasa mikoani ili kutoa
fursa sawa kwa watanzania kupata hati za ardhi yao.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment