November 03, 2016


 Hali ya sintifahamu, imezuka leo mkoani Morogoro, kufuiatia tukio la wafanya biasahara ndogondogo maarufu kama wamachinga, kufunga barabara ya Madaraka Road na kisha kuwasha moto katikati ya barabara. Tukio hilo limeibuka baada ya wafanya biashara hao kutawanywa katika eneo eneo hilo lilipokuwapo soko kuu la Mkoa wa Mororgro, kabla ya kuvunjwa ili kupisha ujenzi mpya wa soko la kisasa. Hapo awali Almashauri ya manispaa iliwataka wafanya biasahara katika soko hilo, kuondoka ili kupisha ujenzi wa soko hilo unaotarajiwa kuanza muda wowote. Baadi ya wafanya biashara walitii amri hiyo na kwenda katika eneo walilopangiwa la Manzese na Kikundi, lakini baadhi yao waligoma na kuendelea na biashara nje ya eneo la soko hilo lililobomolewa. 
 
 Mara kwa mara wafanya biashara hao walitangaziwa kuondoka katika maeneo hayo lakini walionekana kupinga na kuendelea na zoezi hilo, ndipo mapema leo hii Mgambo wa manispaa walipofika kuwataka waondoke, ndipo zikatokea purukushani mpaka jeshi la polisi kuingilia kati kwa kufyatua mabomu ya machozi ili kuwatawanja. Lakini bada ya kutawanyika na polisi kuondoka, ndipo hali ikabadilika na wafanya biashara hao kuamua kufunga barabara ya Madaraka kwa kupanga mawe, matofali na kuwasha moto mkubwa uliozua kero kwa wengine na vyombo vya usafiri kushindwa kupita kwa muda. Muda mfupi baadaye jeshi la polisi likafika  na kuzibiti tukio hilo.



Related Posts:

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE