Chama cha ACT Wazalendo kimepinga utaratibu wa sasa wa utoaji mikopo
wa elimu ya juu ambao wanasema ukiachwa bila kupingwa utasababisha
watoto wengi wa maskini washindwe kujiunga na elimu ya juu kwa kukosa
mikopo.
Akizungumza na waandishi wa habari Alhamisi hii,Katibu wa Itikadi,
Mawasiliano na Uenezi wa ACT, Ado Shaibu, amesema chama hicho kimetoa
tamko hilo, baada ya takwimu zilizotolewa hivi karibuni na Bodi ya
Mikopo kwa Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HELSB) kuthibitisha kuwa takribani
wanafunzi 65,000 wenye sifa za kujiunga na elimu ya juu, ni wanafunzi
20,000 ndiyo waliopata mikopo.
“Kwanza tulitaka tulitilie mkazo sana suala la watoto maskini
kutelekezwa kwenye ugawaji wa mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu.
Kwenye mikoa mingi tuliyotembelea viongozi wa chama wamepinga vikali
utaratibu wa sasa wa utoaji mikopo wa elimu ya juu ambao kama ukiachwa
bila kupingwa utawafanya watoto wengi kutoka familia washindwe kujiunga
na elimu ya juu. Hali hii imethibitishwa na takwimu iliyokwishatolewa na
bodi ya mikopo”,amesema Shaibu.
“Kwenye mikoa mingi iliyotembelewa viongozi wa chama wamepinga vikali
utaratibu wa sasa wa utoaji mikopo wa elimu ya juu ambao kama ukiachwa
bila kupingwa utafanya watoto wengi kutoka familia maskini washindwe
kujiunga na elimu ya juu kwa kukosa mikopo,” ameongeza.
BY: EMMY MWAIPOPO
0 MAONI YAKO:
Post a Comment