
Staa wa muziki kutoka Nigeria, Yemi Alade ambaye yupo nchini kwa sasa kwa ajili ya tamasha la Fiesta Dar 2016, ameeleza jinsi alivyoweza kuimba wimbo kwa Kiswahili ambao aliupa jina la Na Gode-Swahili Version’.
Akizungumza na waandishi wa habari kabla ya kufanyika kwa Fiesta, Yemi Alade amesema anapenda kujifunza lugha mbalimbali ikiwemo kiswahili na alipotaka kuimba wimbo huo haikumpa shida sana kukamilisha nyimb nzima.
“Napenda kufahamu lugha nyingi, nina nyimbo nilizoimba kwa kifaransa, kireno zote hizo nimejifunza kutoka kwa watu niliokutana nao, najifunza lugha kutoka kwa marafiki nafikiri this time Vanessa [Mdee] atanifundisha Kiswahili,” alisema Yemi Alade.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment