Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda amesema Kaimu Mganga Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Bakari Mbwana hawezi kupandishwa cheo kuwa Mganga Mkuu wa Wilaya hiyo mpaka hapo atakapotatua changamoto zahanati ya Tundu Songani Kata ya Pemba Mnazi.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda akiwauliza wananchi kuhusu utendaji wa Mganga Mkuu wao.
Makonda aliyasema hayo katika ziara yake ya siku ya pili Wilayani Kigamboni wakati alipokwenda kuzindua madarasa ya Shule ya Msingi Tundu Songani,ambapo mara baada kuzindua madarasa hayo aliongea na wananchi na kusikiliza kero.
“Kwa mamlaka uliopewa na Rais wewe ndio mwakilishi wake katika upande wa afya wilaya ya Kigamboni huwezi kupandishwa cheo kuwa Mganga wa Wilaya hii mpaka hapo utakaponihakikishia uwezo wako wakufanyakazi”alisema Makonda.
Makonda alisema hawezi kumtumbua jipu Mganga huyo kwa kuwa ameteuliwa muda mfupi mpaka sasa ana mwezi mmoja hivyo amempa muda kwa ajili ya kumwangalia katika utendaji wake kama kaimu Mganga mkuu wa Wilaya hiyo.
Hatua hiyo ya Makonda kutoa agizo la kumchunguza Mganga huyo limetokana na wananchi wa Tundu Songani kulalamika mbele ya Serikali ya Mkoa kuwa mganga huyo hajawai kufika eneo hilo na wananchi kupewa lugha chafu wanapokwenda katika zahanati .
Kwa upande wake Kaimu Mganga Mkuu huyo,alipoulizwa kuhusiana na malalamiko ya wananchi alisema yeye kama mganga mkuu anachofahamu changamoto iliyokuwepo katika zahanati hiyo ni gari la wagonjwa akuna.
Naye Mwananchi Asha Abadalah alisema mwanamke mjamzito akienda katika kituo hicho anaambiwa aende katika hospitali ya Wilaya ya Temeke na Mgaga huyo hajawai kufika katika Kata hiyo ya Pemba Mnazi ni mara yake ya kwanza.
Wakati huohuo katika hatua za kusogeza huduma za jamii kwa wananchi hao,Makonda aliwataka wananchi kuchangamkia mradi wa umeme vijijini (REA) kwa gharama ya sh,27,000.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment