Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa mamlaka ya mapato nchini TRA,
Bernard Mchomvu ameamka na habari mbaya Jumapili hii. Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Dkt John Magufuli amemshushia rungu yeye na bodi
yake. Hiyo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ikulu Jumapili hii:
Hatua hiyo imekuja katika kipindi ambacho mamlaka hiyo imeonesha
kufanya vizuri zaidi katika kukusanya mapato ambapo imefanikiwa
kukusanya shilingi trilioni 1.15 kwa mwezi Oktoba mwaka huu ikiwa ni
kukamilisha malengo waliyojiwekea katika ukusanyaji wa mapato.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment