Mshambuliaji wa Real Madrid na timu ya Taifa ya Ureno, Cristiano Ronaldo amemshinda hasimu wake wa karibu, Lionel Messi na kutwaa tuzo ya Ballon d’Or kwa mara ya nne. Cristiano Ronaldo (31) aliisaidia klabu yake ya Real Madrid kutwaa kombe la Klabu Bingwa Ulaya huku akiifungia timu yake ya taifa magoli matatu na kuiwezesha kutwaa Kombe la Ulaya (EURO 2016). Mataji mengine ya Ballon d’Or alishinda mwaka 2008, 2013 na 2014. Kwa sasa Ronaldo amepitwa na Messi kwa tuzo moja ambaye amelitwaa mara tano yaani mwaka 2009, 2010, 2011, 2012 na 2015.
Tuzo hiyo hupewa mchezaji bora wa Ulaya kulingana na kura 173 zinazopigwa na waandishi wa Habari kutoka Duniani kote
Ronaldo: "So happy and glad to win. Thanks Real Madrid and Portugal National team.amazing year.
Simmmmmmm💪🏽💪🏽💪🏽💪🏽"
0 MAONI YAKO:
Post a Comment