December 09, 2016


Mkurugenzi Mtendaji wa Makampuni ya Mohammed Enterprises Tanzania Limited (MeTL Group), Mohammed Dewji ametunukiwa tuzo ya Mjasiriamali Bora kwa mwaka 2016 wa Afrika.



Dewji ametajwa kuwa mshindi wa tuzo hiyo na Shirikisho la Wafanyabiashara wa Ufaransa (MEDEF) kutokana na biashara ambazo anazifanya katika nchi mbalimbali Afrika na jinsi ambavyo vinasaidia kuleta maendeleo.
Akizungumza baada ya kutangazwa kuwa mshindi, Dewji alieleza jinsi ambayo amefurahishwa na ushindi wa tuzo hiyo na kutumia nafasi hiyo kuelezea mipango ambayo ameipanga kuifanya kupitia kampuni yake ya MeTL ya kusaidia bara la Afrika kupata maendeleo kupitia sekta binafsi.
“Ili kuwe na maendeleo endelevu ya muda mrefu na ambayo yatahakikisha sekta binafsi zinafanya vizuri Afrika, katika kufanikisha hilo, makampuni binafsi yanatakiwa kuwahusisha na watu masikini wakianza na wazalishaji, wauzaji, wafanyakazi na wateja na hivyo ndivyo MeTL Group inavyofanya Tanzania,” alisema Dewji.

Pamoja na kuzungumza kuhusu tuzo aliyoipata, pia Dewji alitumia nafasi hiyo kuwashawishi wafanyabiashara wa Ufaransa kufanya uwekezaji katika nchi za Afrika Mashariki kwani zinakuwa kwa kasi na kuna utulivu wa kisiasa jambo ambalo linaweza kuwasaidia kufanya biashara zao kwa mafanikio makubwa.
Aidha Dewji alizungumza kuhusu utendaji kazi wa Rais wa Tanzania, Dk. John Magufuli kwa juhudi zake za kupambana na vitendo vua rushwa kwa watumishi wa Serikali na kuongeza nguvu zaidi katika mambo ya  maendeleo.
czf9qlqwqaaxxu4

Tuzo aliyoshinda Mohammed Dewji 

Katika ukurasa wake wa Instagram Mo ameandika haya.

  Moodewji: Jana nimeshinda tuzo ya "mjasiriamali wa mwaka  -Afrika" iliyotolewa na MEDEF nchini Ufaransa . Ninashukuru sana kwa zawadi hiina ninafurahi kupeperusha vyema bendera ya nchi yangu TZ .Asante wote #UmojaniUshindi 

Ameandika mkurugenzi wa METL Tanzania Mohammed Dewji

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE