Bunge la Cuba limepitissha msuada wa sheria unaopiga marufuku kutumia jina la Fidel Castro katika majengo, mitaa na minara ya kihistoria nchini humo.
Fidel Castro alifariki Novemba 25 akiwa na umri wa miaka 90.
Rais wa Cuba Raul Castro alifahamisha Fidel Castro alikataa katika uhai wake kutumia jina lake na kupelekea suala hilo kuwasilishwa katika baraza la bunge la Cuba.Msuada huo wa sheria unapiga marufuku matumia jina au picha ya kiongozi wa kihistoria wa Cuba katika barabara au majengo ya umma nchini humo.
Hakuna taarifa iliotolewa kuhusu adhabu kwa yeyote atakae kiuka sheria hiyo.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment