Watu zaidi ya 30 wamefariki katika baada ya kushambuliwa kwa silaha mjini Istanbul nchini Uturuki. Shambulizi hilo la silaha limetekelezwa katika mkesha wa mwaka mpya. Shambulizi hilo limetekelezwa katika mgahawa wa Ortaköy unaopatikana katika mji wa Istanbul.
Watu 39 wameripotiwa kufariki na wengine 69 kujeruhiwa katika shambulizi hilo. Mtu mmoja aliekuwa kavalia mavazi ya "Father Christmas" alifyatua risasi na kusababisha maafa hayo. Vasıp Şahın kiongozi wa Istanbul alifahamisha kuwa mtu alifyatua risasi akşwalenga askari walinda usalama waliokuwa wakilinda usalama katika mgahawa huo katika mkesha wa mwaka mpya.Waziri wa mambo ya ndani wa Uturuki Süleyman Soylu amesema kuwa operesheni kali ya kumsaka alieendesha shambulizi hilo imeanzishwa koti mjini Istanbul. Miongoni mwa watu waliofariki katika shambulizi hilo wamo wageni 16.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment