February 05, 2017

Benki ya KCB Tanzania imeendesha mafunzo ya siku tatu kwa Wanawake Wajasiriamali Mkoani Morogoro ambapo mafunzo hayo ya siku tatu yaliyojulikana kama 2JIAJIRI ambapo yatakuwa chachu kwa Wanawake hao kujikwamua na hali ya kiuchumi na maisha katika shughuli zao ndogondogo.
Meneja wa Tawi la Morogoro wa Benki ya KCB Tanzania Emmanuel Mnzava, akizungumza na wanawake wajasiriamali waliohudhuria semina ya mafunzo ya siku tatu kwa ajiri ya wanawake wajasiriamali inayoitwa 2JIAJIRI iliyoandaliwa na benki hyo jijini Morogoro
Mwalimu wa Ujasiriamali wa Kituo cha Uwezeshaji na Ushindani Tanzania (TECC) Grace Makoye akitoa mafunzo ya ujasiriamali yaliyoandaliwa na Benki ya KCB Tanzania kwa wanawake wajasiriamali wa mkoa wa Morogoro.
Mwalimu wa Ujasiriamali wa Kituo cha Uwezeshaji na Ushindani Tanzania (TECC) Allen Mhidze akitoa mafunzo ya ujasiriamali yaliyoandaliwa na Benki ya KCB Tanzania kwa wanawake wajasiriamali wa mkoa wa Morogoro.
Baadhi ya wanawake wajasiriamali waliohudhuria mafunzo ya ujasiriamali yaliyotolewa na Benki ya KCB mkoani Morogoro.
Meneja wa Tawi la Morogoro wa Benki ya KCB Tanzania Emmanuel Mnzava, (aliyekaa katikati) na afisa biashara wa benki ya KCB tawi la morogoro, Lela Kisinda (aliyekaa kulia) wakiwa kwenye picha ya pamoja na wanawake wajasiriamali waliohudhuria na kumaliza mafunzo ya ujasiriamali yalitolewa na benki hiyo katika mkoa wa Morogoro

Related Posts:

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE