March 12, 2017

 

Mbunge wa Nzega Mjini Hussein Bashe amefunguka mazito leo asubuhi kuhusiana na sakata la timua timua linaloendelea dhidi ya wanachama wasaliti ndani ya CCM hukoMjini Dodoma katika Mkutano Mkuu Maalum wa chama hicho  .
Mbunge huyo amesema hawezi kuwa na hofu ya aina yeyote kwa kuwa hana jambo baya alilolifanya ndani ya chama hicho hivyo hawezi kuteteleka na wanaotimuliwa wanachama.
“Sina hofu na timua timua ya wanachama wasaliti kwasababau naamini wamefanya maamuzi kwa kupitia mchakato ndani ya chama, kwa hiyo sina hofu kwasababu chama chetu kinaongozwa na katiba pamoja  na kanuni zilizopo unakuwa na hofu pale unahisi kuna jambo umelifanya kinyume na taratibu”-Alisema Bashe 

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE