March 09, 2017

 

Baadhi ya wagombea wa nafasi ya  urais kupitia kwa chama cha wanasheria wa Tanganyika TLS wanatarajia kuwasilisha maombi ya kujumuishwa kama wadaiwa katika kesi ya kupinga kufanyika kwa uchaguzi wao uliopangwa kufanyika tarehe 18  ya mwezi huu
Wamefikia hatua hiyo ili kuuongezea nguvu upande wa wadaiwa kufuatia kesi iliyofunguliwa na wanachama wawili wa chama hicho ambao wamefungua kesi katika mahakama kuu kupitia mkoa wa Dodoma na Dar es salaamu .
Wakizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam leo mgombea TUNDU LISSU amesema uchaguzi huo umekuwa ukifuatiliwa kwa karibu na watu wengi huku akibainisha kuwa kuna kile alichokiita njama dhidi ya kuuharibu uchaguzi huo
Lissu ameongeza kuwa wanachama wa chama hicho hawatakuwa tayari kuona uchaguzi unasitishwa kutokana na sheria za chama hicho kusisitiza kufanyika kwa uchaguzi wa chama hicho ambacho amedai kimekuwa na mchango mkubwa katika tasnia ya sheria nchini.
Katika kesi ya msingi ya kupinga uchaguzi huo iliyofunguliwa na wanachama hao, washtakiwa ni mwanasheria mkuu wa serikali pamoja na chama chenyewe (TLS).

Kwa upande wake mgombea mwingine wa nafasi ya urais ambaye aliwahi kuwa waziri wa mambo ya ndani  mheshimiwa LAWRENCE MASHA amebainisha kuwa chama chao hakina kipengele chochote kinachozuia wanasiasa kugombea nafasi ya uongozi katika chama hicho huku akiwataka wanachama wa chama hicho kujitokeza kwa wingi kwenye mkutano mkuu wa chama hicho ambao unatarajiwa kufanyika mkaoni Arusha siku ya tarehe 18 ya mwezi huu

Related Posts:

  • PAPA AWASILI UFILIPINO Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani,Mtakatifu Francis, amewasili nchini Ufilipino, nchi yenye Wakatoliki wengi zaidi barani Asia, huku ulinzi mkali ukiwa umeimarishwa. Maelfu ya Wafilipino wamejipanga katika misur… Read More
  • NEW VIDEO: KIBOKO YANGU- MWANA FA ft ALLY KIBA Hii ni video mpya ya mkali Hamisi Corleone Mwinjuma aka Mwana FA ya Kiboko yangu ni moja kati ya ambazo zimekuwa zikisubiriwa kwa hamu na watu wengi. Video imetayarishwa na Director Kelvin Bosco wa … Read More
  • RONALDO DE LIMA KUREJEA DIMBANI Ronaldo de Lima anavyoonekana sasa. Mshambuliaji wa zamani wa timu ya taifa ya brazil Ronaldo Luís Nazário de Lima anatarajia kurejea tena dimbani. De lima ameahidi kupunguza… Read More
  • WATANZANIA WENGI WAFUNGWA HONG KONG Kasisi mmoja raia wa Australia amefichua na kuthibitisha kuwa kuna idadi kubwa ya wafungwa wenye asili ya Afrika katika magereza ya Hong Kong, wengi wao wakiwa ni kutoka Tanzania. Kasisi huyo John Wortherspoon ambaye … Read More
  • MARKEL: TUTAWALINDA WAYAHUDI NA WAISLA,U UJERUMANI Kansela Angela Merkel   Kansela wa Ujerumani, Angela Merkel ameahidi kuwalinda Wayahudi na Waislamu wanaoishi nchini Ujerumani dhidi ya ubaguzi. Amesema demokrasia ndiyo njia bora ya kupambana na machafuko yanayo… Read More

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE