March 06, 2017


HATIMAYE Tundu Lissu, Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki, ameachiwa kwa dhamana na Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam baada ya kufutiwa mshitaka na kukamatwa tena leo asubuhi kwa tuhuma za kufanya uchochezi wa kidiniLissu alikamatwa akiwa ndani ya Mahakama ya Kisutu baada ya serikali kuwasilisha taarifa kuwa haina nia ya kuendelea na kesi iliyofungua hapo awali na kisha polisi kumpeleka kituo ch kati kwa mahojiano.Taarifa zilizopatikana leo jioni zinaeleza kuwa Lissu amehojiwa juu ya kauli yake aliyoitoa katika uchaguzi mdogo wa Jimbo la Dimani, Zanzibar miezi miwili iliyopita pale alipotamka kuwa “Uchaguzi w Zanzibar ulikuwa haramu kama muislam kula nyama ya nguruwe.”Mapema leo asubuhi baada ya kukamatwa Lissu alindika ujumbe ukisema, anaamini kukamatwa kwake kuna uhusiano wa moja kwa moja uchaguzi ujao wa Chama cha Mawakili hapa nchini (TLS), unaotarajia kufanyika wiki mbili zijazo.

Related Posts:

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE