Dunia, leo inaadhimisha siku ya wanawake Duniani, Wanawake mbalimbali na jamii kwa jumla wamejikita katika mambo mbalimbali ya kijamii kwa lengo la kuiadhimisha siku hii kwa kumbukumbu muhimu.
Kwa upande wake, mrembo wa Tanzania asiyehisha utamu ambaye kwa hivi sasa ni mwana chama wa CHADEMA Wema Sepetu amejiunga na wanawake wengine mkoani Morogoro katika zoezi la kupanda miti, ikiwa ni sehemeu ya maadhimisho hayo. Wema aliungana na Mbunge wa Viti Maalum CHADEMA Devotha Minja na wanawake wengine katika zoezi hilo
Muigizaji huyo amedai upandaji wa miti utakuja kuwa tija kwa jamii hasa hasa kupunguza kero kubwa ya maji inayotukabili wanawake.
“Leo ni siku ya wanawake Duniani, na kama mwanamke nikaonelea nijiunge na wanawake wenzangu wa Mkoa wa Morogoro siku ya leo katika upandaji wa miti ambao utakuja kuwa tija kwetu na kupunguza kero kubwa inayotukabili ya Maji,” aliandika katika ukurasa wake wa Instagram
0 MAONI YAKO:
Post a Comment