April 14, 2017

 
 Shirikisho la soka duniani, FIFA na lile la Afrika, CAF kwa pamoja wameupitisha uwanja wa CCM Kirumba uliopo jijini Mwanza, kutumika kwenye mechi za kimataifa.Hatua hiyo imetangazwa Ijumaa hii na Rais wa shirikisho la soka Tanzania, TFF, Jamal Malinzi. “Wana Mwanza hongereni Uwanja wa CCM Kirumba umepitishwa na CAF na FIFA kutumiwa kwa mechi za Kimataifa,” ametweet Malinzi.
Kupitishwa kwa uwanja huo kumekuja baada ya wataalamu wa Ufundi wa CAF kwenda Mwanza kuukagua uwanja huo mwishoni mwa mwaka jana.
Viwanja vingine ambavyo CAF na FIFA inavitambua nchini hadi sasa ni Amani wa Unguja, Zanzibar, Azam Complex na uwanja wa taifa wa Dar es Salaam.
Kupitishwa kwa CCM Kirumba kuna maana kuwa sasa mechi kubwa kama vile fainali za Kombe la Shirikisho, Ngao ya Hisani pamoja na mechi kubwa za kimataifa za kirafiki na mashindano ya CECAFA, CAF na FIFA ruksa kufanyika huko.
Viwanja vingine ambavyo vimekaguliwa na vinasubiri kupitishwa ni Gombani ulioko Pemba; Sokoine wa Mbeya na Kaitaba wa Kagera.
 
 
 

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE