Kamati ya Katiba, Sheria na Hadhi za Wachezaji ya TFF imeshindwa kuamua
suala la Simba na Kagera Sugar kuhusu point 3 za kagera ilizopewa Simba,
baada ya malalamiko ya malalamiko kuwa Kagera walimchezesha mchezaji
kinyume na kanuni.
Kamati
hiyo ambayo imekaa leo, imeshindwa kufikia muafaka licha ya kuwepo kwa
sehemu kubwa ya waliohusika na mchezo kati ya Kagera Sugar na African
Lyon, ambao ndiyo mchezo unaobishaniwa kuwa mchezaji Mohamed Fakhi
alipewa au hakupewa kadi ya njano.
Baadhi ya wahusika hao ni pamoja na
viongozi wa timu zote tatu (Kagera, Simba na African Lyon), waamuzi wote
wa mchezo ule, mchezaji mwenyewe wa Kagera Mohamed Fakhi na wengineo
Kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa TFF,
Celestine Mwesigwa, Kamati hiyo inahitaji ushahidi zaidi ili kulimaliza
suala hilo, na amesema kikao kingine kitafanyika kesho Jumatano Aprili
19 kuanzia saa 6 mchana.
"Hili suala hi la kisheria
kwahiyo linahitaji ushahidi zaidi, kuna watu wanadhani kamati hii inakaa
ili kupindua maamuzi ya kamati ya saa 72, lakini kimsingi jukumu la
kamati hii ni kutafsri sheria siyo kubadili maamuzi ya kamati nyingine" Amesema Mwesigwa
Mwesigwa amesema pia kuwa kikao hicho
kimejadili suala la mchezaji wa Ludovic Venance aliyelalamikiwa kuwa na
utata kwenye usajili wake katika klabu ya African Lyon, ambapo amesema
kamati imemuidhinisha mchezaji huyo kuchezea African Lyon akitokea Mbao
FC.
Amesema Kamati hiyo imebaini kuwa
usajili wake ulikuwa na utata uliosababishwa na baadhi ya viongozi ambao
watachukuliwa hatua huku timu ya African Lyon ikipigwa faini ya
shilingi laki 5.
Mwesigwa hajazungumzia malalamiko ya
Yanga ya kudai ushindi wa mchezo uliowakutanisha wao na African Lyon
ambao mchezaji huyo alicheza, na baadaye Yanga kulalamika kuwa Ludovic
hakuwa mchezaji halali wa Africa Lyon.
Katika mchezo huo, Yanga ilitoka sare ya bao 1-1 na African Lyon
0 MAONI YAKO:
Post a Comment