Kwa mara ya kwanza wakazi wa Mji wa Dodoma wanatarajia kushuhudia mubashara sherehe za Muungano wa Tanganyika na Zanzibar Aprili 26 mwaka huu katika uwanja wa Jamhuri.Sherehe hizo kufanyika Dodoma mwaka huu ni zimeambatana na serikali kuhamishia makao makuu yake mjini humo, na pia ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ambaye ndiye atakayekuwa mgeni Rasmi.
Taarifa kutoka kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Ajira, Kazi, Vijana na Watu Wenye Ulemavu Jenista Mhagama imesema kuwa sherehe hizo zitapambwa na maonesho ya ukakamavu na mbinu za medani katika kupambana na maadui hasa kulinda amani ya nchi kutoka kikosi maalum cha Makomandoo wa Jeshi la Wanachi Tanzania (JWTZ).
0 MAONI YAKO:
Post a Comment