April 09, 2017

Image result for malisa gj 


Image result for roma mkatoliki na moni 
ROMA na Moni

Hili la Roma limenifundisha jambo moja kubwa. Maana halisi ya UNAFIKI.!! Wanasiasa walewale ambao hawajawahi kutoa hata sentensi moja juu ya kupotea kwa Ben miezi mitano sasa, ndio wapo mstari wa mbele kuzungumza kuhusu Roma. Unafiki.!! Polisi walewale waliopewa mawasiliano yote ya Ben na watu aliowasiliana nao wameshindwa kutrack watu hao lakini wameweza kwa Roma. Unafiki.!! Vijana walewale wa CCM waliosema Ben hajatekwa, ndio haohai walioshinda mitandaoni kutuambia Roma katekwa. Unafiki.!! Vijana walewale wa CCM waliolibeba suala la Ben kisiasa (na kusema ni filamu) ndio haohao walikua mstari wa mbele kusema tusilibebe suala la Roma kisiasa. Unafiki.!!

Image result for ben saanane Ben Saanane


Simaniishi hatukupaswa kumtafuta Roma. Namaanisha tumechangia kumpoteza Ben kwa sababu ya Unafiki. Roma amepatikana kwa sababu ya SOLIDARITY iliyooneshwa. Kuanzia kwa wasanii wenzie, familia, ndugu, jamaa, marafiki, wadau wa sanaa na wanasiasa pia. Japo Roma hakua mwanasiasa lakini wanasiasa wamevalia njuga sana suala lake.
Lakini Ben alitelekezwa. Kuanzia na wanasiasa wenzie na hata "watu wake wa karibu" waliopaswa kuwa mstari wa mbele kumpigania, kumtetea, kumlilia na kushinikiza watekaji kumuachia. Ilibaki sauti ya familia na marafiki wachache ambayo possibly haikuwatisha watekaji. Ben ni mhanga wa kutelekezwa. Miezi mitano ya kupotea kwake watu wanaona ni kawaida. Natamani mshikamano huu tuliouonesha kwa Roma tungeuonesha pia kwa Ben, nina hakika angeshapatikana..!!
#BringBackBenAlive.!

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE