April 19, 2017

 Image result for simu find my iphone

Mshukiwa wa wizi ambaye inaaminika alikuwa ameiba zaidi ya simu 100 aina ya iPhones amekamatwa nchini Marekani.
Mwizi huyo alikamatwa baada ya watu waliokuwa wameibiwa simu zao kutumia programu tumishi ya Find My iPhone kufuatilia simu zao.
Simu hizo zilikuwa zimeibiwa katika tamasha la muziki la Coachella katika jimbo la California, polisi wamesema.
App hiyo huonesha ilipo simu ya mtu, na baada ya watu waliokuwa wameibiwa simu zao kupiga ripoti kwa polisi, maafisa walifuatilia kwa kutumia app hiyo hadi wakamnasa mshukiwa.
Walipata zaidi ya simu 100 zikiwa kwenye mfuko wa mshukiwa huyo wa wizi.


Baadhi ya simu zilirejeshewa wenyewe papo hapo.
Nyingine zimekabidhiwa kwa wasimamizi wanaokusanya mali na bidhaa zilizopotea wakati wa tamasha hilo.
Polisi walikuwa tayari wametumwa kwa wingi katika tamasha hilo baada ya visa vya wizi wa simu kuongezeka, anasema afisa wa polisi Dan Marshall, akinukuliwa na mtandao wa Gizmodo.
Lakini wenye simu ndio waliosaidia kunaswa kwa mshukiwa.
Wanaohudhuria tamasha hilo wameshauriwa:
  • Kutoweka vitu vyao vya thamani katika mifuko yao ya nyuma
  • Kuhakikisha vitu vyao vya thamani hawaviweki pamoja
  • Kubeba pochi bandia ili kuwahadaa wachopozi

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE