Hivi leo 7th Aprili mamake Kanumba na waliokuwa marafiki wake wakaribu walivyoadhimisha miaka mitano baada ya muigizaji huyo kufariki. Wote waliojitokeza walikutana kwenye makaburi ya kinondoni jijini Dar es salaam kufanya ibada kabla ya kumuwekea marehemu maua.
Ingawa sio wengi waliojitokeza, mama Kanumba aliwashukuru wote waliomsidikiza kwenye maadhimisho hayo. Alisema,
“Kiukweli nawashukuru wote waliojitokeza kwenye shughuri hii ya leo kwani sikuwa nimeandaa kitu kikubwa ila nashukuru mungu kuniwezesha,”
Johari ambaye ni staa wa filamu bongo pia aliwasihi wasanii kupendana na kupeana support kwa kila kitu. Na kulingana na alichosema, muigizaji huyu alikuwa na mengi ambayo yangewafaidi mastaa wa bongo kwa hivi sasa. Johari amesema:
Kila mwaka lazima nimkumbuke Steven Kanumba kwani ndiye alikuwa akinitia faraja na nguvu ya kutokata tamaa katika jambo unaloliamini. Kanumba hakupenda kushindwa kwa kile alichokiamini, hakika pengo lake halitazibika, namwombea huko aliko alale mahali pema peponi, alipigania tasnia ya filamu, sema ndiyo hivyo hakuweza kufikia malengo yake, siwezi kumsahau, nitamkumbuka kwa mengi aliyoniachia.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment