April 19, 2017

Ismail Aden Rage-Mwenyekiti wa zamani wa klabu ya Simba SC
Mwenyekiti wa zamani wa Simba Alhaj Aden Rage ameungana na wadau wengine kupinga matokeo ya mezani kwakua kuna njia nyingi za kuweza kuepuka timu kupewa au kupokwa ushindi mezani.
Rage amesisitiza kwamba, hata walezi wa soka FIFA na CAF pia hawafurahishwi na matokeo ya mezani na wao wamejiwekea taratibu nzuri za kuepuka timu kupewa au kupokwa ushindi mezani.
“FIFA wana-discourage sana ushindi wa mezani, na katika kuhakikisha hilo halitokei, FIFA  na CAF wanashauri kwamba, endapo mchezaji ana kadi tatu za njano au kadi nyekundu afisa wa TFF anapaswa kumwandia barua commissar wa mchezo na klabu inayohusika kwamba mchezi flani hapaswi kucheza kwa sababu ambazo zitatolewa.”
“Kwenye pre-match meeting, commissar ataisoma hiyo barua na klabu husika inaelezwa hii yote ni kwa sababu FIFA wanajaribu kuepuka ushindi wa mezani, kwa hiyo utaona hapa wenzetu wanathamini fair play. Sisi hatufanyi hivyo badala yake tuna viziana kwa kusema kazi ya kuweka kumbukumbu ni ya vilabu kitu ambacho si sawa.”
“Ninasema hivyo kwa sababu nina ushahidi kwa sababu nimeshakuwa match commissar wa CAF na FIFA naletewa barua kabla hata ya kusafiri kwenda mahali ambapo mechi itachezwa, napofika kwenye pre-match meeting nasema kabisa mchezaji fulani hatakiwi kucheza, utakapomchezesha unatafuta kuadhibiwa.”
Rage pia ameshangazwa na Kamati ya Katiba, Sheria na Hadhi za wachezaji kujadili maamuzi ambayo yalishafanywa na kamati ya saa 72 kwa kusema kwamba, kikanuni hawana mamlaka hayo.
“Sualal hili halifai kwenda kwenye kamati ya Katiba, Sheria na Hadhi za wachezaji, sio kazi yao. Kama kuna tatizo lolote ambapo Kagera wanaona hawakutendewa haki wana haki ya kuomba maamuzi kupitiwa lakini chombo ambacho kinatakiwa kufanya hivyo sio kamati ya katiba, sheria na hadhi za wachezaji isipokuwa kamati ya nidhamu.”
“Katika kamati ya nidhamu kuna kitu kingine ambacho nimeona wamefanya makosa, ameitwa fourth official aliyekuwepo kwenye mchezo ambao taarifa yake inatiliwa shaka. Ukisoma kanuni za kamati ya nidhamu inasema kwamba, kama itatokea kusigana kwa taarifa, haitaangaliwa ripoti ya fourth official wala commissar bali ripoti ya referee ni ya mwisho. Ripoti ya fourth official au commissar itaangaliwa kwa matukio ya nje ya uwanja tu.”
“Ukisoma sheria 17 za soka, sheria namba 5(ii) inazungumzia mamlaka ya kutoa maamuzi ya mwisho ni referee. Lakini najaribu kuangalia ni wapi hii kamati ya katiba, sheria na hadhi za wachezaji ina mamlaka ya kupitia sioni kwa hiyo nasema katika hili TFF wamekosea.”
“Kamati ya mwisho ya kumaliza ilikuwa ni ileile ya saa 72 tena huruhusiwi hata kukata rufaa kwa sababu adhabu ni ya moja kwa moja kikanuni.“

Source: shaffihdauda.co.tz

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE