April 10, 2017

 

Kukithiri kwa uvamizi na watu maarufu kutekwa, baadhi kutoweka na wengine kuibuliwa siku chache baadaye, kumesababisha Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe (ACT-Wazalendo) kuamua kupeleka suala hilo bungeni.

 Zitto alisema jana kuwa amepata taarifa za kushtua hivyo atalipeleka suala hilo bungeni, huku  mwenzake wa Arusha Mjini, Godbless Lema akimtaka Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba ajiuzulu.

  Matukio yaliyoibua mjadala huo ni kutekwa na baadaye kuachiwa kwa msanii wa hiphop, Roma Mkatoliki na wenzake wanne, kuvamiwa kwa Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye (CCM) na kuvamiwa kwa studio za televisheni za Kampuni ya Clouds Media.

 Pia, matukio hayo yamesababisha kukumbukwa kwa tukio la kutoweka kwa Ben Saanane, ambaye alikuwa msaidizi wa Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe.

 Zitto alisema ana taarifa za kushtua kuhusu kupotea kwa Saanane, taarifa ambazo alisema ni Bunge pekee linaloweza kuzithibitisha, hivyo anaandaa hoja binafsi atakayoiwasilisha ndani ya chombo hicho cha kuisimamia Serikali wakati wowote. Kwa sasa, Bunge linaendelea na vikao vyake vya bajeti mjini Dodoma.

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE