
Meneja
Uwakala wa Benki NMB, James Wanyama (kulia) akifafanua jambo kwa
waandishi wa habari walipokuwa wakizinduwa huduma za
NMB Wakala zilizoboreshwa zaidi zenye gharama nafuu. Kushoto ni Mkuu wa
Idara ya Huduma Mbadala za Kibenki wa NMB, George Kivaria. Kwa huduma
hizo mteja wa NMB anaweza kuweka na kutoa fedha mtaani kwake, kuangalia
salio na hata kufanya malipo ya tozo mbalimbali akiwa katika mawakala wa
NMB popote alipo.
UPATIKANAJI
wa huduma za Benki ya NMB umezidi kuboreshwa na sasa umesogezwa zaidi
mtaani kwako. Mteja wa NMB na asiyekuwa mteja kupitia huduma ya NMB
Wakala sasa anaweza kuweka kutoa fedha na hata kulipia huduma mbalimbali
akiwa mtaani kwake bila ya uhitaji wa kufika katika tawi la benki ya
NMB.
Akizungumza
leo jijini Dar es Salaam na waandishi wa habari alipokuwa akitambulisha
huduma hiyo iliyoboreshwa zaidi, Mkuu wa Idara ya Huduma Mbadala za
Kibenki wa NMB, George Kivaria alisema kuboreshwa kwa huduma hiyo sasa
kunawawezesha wateja kupata huduma za benki hiyo kwa haraka na kwa
usalama na uhakika popote walipo.
Alisema
huduma hiyo pia inamwezesha mteja wa NMB kuweza kuweka fedha, kutoa,
kujua salio lake kwa gharama nafuu zaidi, huku ikitolewa na mawakala
zaidi ya 2000 ambao wanapatikana maeneo mbalimbali ya nchi ikiwemo
maeneo ya vijijini.
Alisema
lengo la NMB ni kusogeza huduma zake karibu zaidi na wateja ili
kurahisisha upatikanaji wa huduma zake tena kwa gharama nafuu. Alisema
huduma zingine ambazo wateja wengine hata wasiokuwa na akaunti
za NMB wanaweza kufanya kwa mawakala hao ni pamoja na kulipa ada za
shule, kulipia tozo za luku, ving’amuzi, malipo ya TRA, leseni na bili
za maji.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment