Producer mkongwe wa muziki kutoka Bongo Record, P-Funk Majani amemtaka
rapa mkongwe Afande Sele kumuandikia mashahiri msanii Hamorapa
anayechipukia kwenye game ili kutimiza ndoto zake na siyo kumkatisha
tamaa.
Mtayarishaji huyo ambaye hivi karibuni alilitambulisha kundi lake
jipya Bongo Los, amelazimika kumuomba Afande kufanya kazi hiyo baada ya
kumdiss Harmorapa kwa kudai ”Harmorapa siyo msanii na hataweza kudumu
kwenye ‘game’ ya bongo Fleva kwa muda mrefu”.
“Afande namuomba kitu , kama unaona dogo anayumba hutakiwi kumbeza
bali unapaswa kumuandikia mashahiri na kukuza sanaa yake. Wewe ni Mfalme
wa Rymes unapaswa kuwasaidia wadogo zako ambao wanaonyesha juhudi zao
binafsi za kujituma. Siyo lazima Afande ufoke wewe usikike wasaidie hawa
wachanga wainuke wawe bora kama wewe usiwakatishe tamaa ukiwa wewe ni
kaka yao,” Majani alikiambia kipindi cha Planet Bongo cha EA Radio.
Aidha Majani ameongeza kwamba Harmorapa amebadilika kimuziki tofauti
na alivyoanza hivyo ni vyema akazidi kupatiwa misaada mbalimbali ya
kumkuza kipaji chake, huku akimwelezea ni kijana anayejituma, mwenye
adabu, pia mwenye shauku ya kufika mbali kimuziki.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment