Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan amewasili mjini Unguja – Zanzibar
akitokea mkoani Dodoma ambapo hapo kesho anatarajiwa kuzindua ya kampeni
maalum inayojulikana kama Mimi na Wewe mjini Unguja.
Lengo la kampeni hiyo ni kuhamasisha
jamii kuchangia kwa hali na mali katika uboreshaji wa huduma mbalimbali
za kijamii ikiwemo elimu, afya, mazingira na kusaidia watu wasiojiweza
katika Mkoa wa Mjini Magharibu, Unguja.
Katika uwanja wa ndege wa Zanzibar,
Makamu wa Rais amepokelewa na Mkuu wa mkoa wa Mjini Magharibi Unguja
Ayoub Mohamed Mahmoud pamoja na Viongozi Mbalimbali wa Serikali na wa
Vyama vya siasa.
Imetolewa na Ofisi ya Makamu wa Rais waJamhuri ya Muungano wa Tanzania, Unguja- Zanzibar20-May-2017
Makamu
wa Rais akipokelewa na Mkuu wa mkoa wa Mjini Magharibi Unguja, Ayoub
Mohamed Mahmoud pamoja na Viongozi Mbalimbali wa Serikali na wa Vyama
vya siasa





0 MAONI YAKO:
Post a Comment