May 13, 2017

 

Mjumbe wa kamati kuu ya CHADEMA na aliyekuwa Waziri Mkuu, Mh. Edward Lowassa amelaani vikali kitendo cha serikali ya Mkoa wa Dar es salam kuzuia kongamano la demokrasia lililopangwa kufanyika siku ya leo may 13, Mnazi mmoja jijini Dar es salaam. 
Mhe. Lowassa leo akizungumza na wanahabari ofisini kwake Mikocheni, Dar amesema kuwa amesikitishwa sana na serikali kuzuia kongamano ambalo lilikuwa na nia njema ya kuzungumza kuhusu demokrasia na kujifunza kutoka kwa watu mbali mbali jinsi ya kufanya siasa bila kukosea na kurekebishana penye makosa.
Mjumbe huyo ameendelea kufafanua kwamba hakuna tatizo kwa vyama vya siasa kutofautiana mawazo kwani ndiyo demokrasia na ndiyo sababu kubwa  ya waandaji kushirikisha watu wenye taaluma tofauti tofauti katika kongamano hilo.

 "Chadema kwa ujumla tunalaani sana kitendo cha Serikali ya Dar es salaam kuzuia mkutano wa amani wa kuwaunganisha watanzania pamoja kwa kutumia kongamano la demokrasia. Kitendo ambacho kimefanywa leo ni kuminya demokrasia. Nia ilikuwa njema na ndio maana waandaji wa kongamano waliweka picha yangu na kinana tukiwa tunatabasamu hivyo hakuna dhambi kwenye kutofautiana mawazo"- alisema Lowassa.
  

 Hata hivyo Mhe. Lowassa amekitaka chama cha Mapinduzi kutonyayasa upinzani kwa kuwa hawataweza kukaa madarakani muda wote huku akiwatahadharisha wakumbuke vyama vya ukombozi wa Afrika vilivyobaki madarakani ni  ANC na CCM.


Related Posts:

  • AY, FA waenda Kortini Kuna uwezekano mkubwa, AY na Mwana FA wamefungua kesi ya masuala ya ukiukwaji wa haki miliki za kazi zao. Mwanasheria maarufu nchini, Alberto Msando amepost picha Instagram akiwa kwenye mahakamu kuu ya Tanzania a… Read More
  • New Music: Linah – Imani   Msanii Linah ameachia wimbo mpya unaitwa “Imani” umetaarishwa na Producer Nash Designer ni wimbo ambao unaujumbe mzuri sana sikiliza hapa alafu toa maoni yako. … Read More
  • Kutoka katika kurasa za Magazeti ya leo Jumatano 11 Mei 2016     Habari za Asubuhi mpenzi msomaji, karibu katika kurasa za magazeti leo hii. makubwa yaliyoandikwa ni haya                       &n… Read More
  • Tahadhari Kuhusu Makachero FEKI Wa TAKUKURU   Tangu kuanza kwa zoezi la kufuatilia wafanyabiashara wanaoficha sukari kwa agizo la Rais wa Jamhuri ya Tanzania Mh. Dr John Pombe Magufuli, kumekuwa na wimbi la watu wanaojiita “makachero wa TAKUKURU  kuto… Read More
  • Orodha ya Mataifa fisadi zaidi Afrika Mashariki   Baada ya waziri mkuu wa Uingereza David Cameron kunaswa na kamera akiidunisha Nigeria kuwa mafisadi wakuu kote duniani BBC imeamua kuangazia kwa umakini ikiwa matamshi hayo ni ya kweli. Je Nigeria imeorodhes… Read More

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE