Mkurugenzi
wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania,
(TRA), Bw. Richard Kayombo (katikati), akitoa hotuba ya ufunguzi wa
semina ya siku moja ya ujasiriamali na elimu ya kulipa kodi kwa
waandishi wa habari kwenye ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania jijini Dar es
Salaam leo Mei 13, 2017. Kulia ni Mwenyekiti wa semina hiyo, Bi.
Angella Msangi na kushoto ni Afisa Kodi Mkuu wa TRA, Bw.Mwangosi
MKURUGENZI
wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA),
Bw. Richard Kayombo, ameendelea kukanusha kwamba, Mamlaka hiyo
haijamkadiria msanii wa muziki wa kizazi kipya,Nassib Abdul ( Diamond
Platnamuz) kulipa kodi ya shilingi Milioni 400.
Hayo
ameyasema leo Mei 13, 2017 wakati akifafanua hoja mbalimbali kwa
waandishi wa habari wanaoshiriki semina ya siku moja iliyoandaliwa na
TRA ili kutoa elimu ya ulipaji kodi kwa waaandishi na kufanyika kwenye
ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), jijini Dar es Salaam.
“Tuko
kwenye hatua za awali za mazungumzo bado hatujakadiria kodi amnayopaswa
kulipa Diamond, na kwa bahatio nzuri tumekaa naye na bado tuko kwenye
mazungumzo na sio kweli kwamba tumemkadiria shilingi Milioni 400,”
Alisema na kuongeza .
“Tunajaribu
kujua vyanzo vyake vya mapato, lakini hata kama imetokea mtu
umekadiriwa kulipa kodi kwa kiasi Fulani na hujaridhika unayo nafasi ya
kukata rufaa kwa Kamishna Mkuu wa TRA, na ndapo hujaridhika na rufaa
hiyo ipo Mamlaka nhyingine ambayo iko nje ya TRA, Tax Tribunal, na bodi
ya Rufaa za kodi.” Alifafanua Bw.Kayombo.
“Hivyo
mtu asiwe mnyonge anayo nafasi ya kukata rufaa, tatu ndani ya TRA, na
mbili nje ya TRA ikiwa ni pamoja na Mahakamani, kwa hivyo watu
wasiogope. Alisema. Awali akifungua semina hiyo. Bw. Kayombo aliwaasa
waandishi wa habari kujenga uzalendo kwa kuunga mkono juhudi za Mamlaka
ya Mapato Tanania TRA, katika kuelimisha umma umuhimu wa kulipa kodi ili
kuiwezesha serikali kutoa huduma stahiki kwa wananchi.
“Najua
kihistoria linapokuja swala la kulipa kodi huwa kuna changamoto nyingi
watu kuelewa swala hili, lakini napenda niwaeleze ndugu zangu, ili
kuiwezesha serikali kutoa huduma stahiki kwa wananchi ni lazima watu
walipe kodi, hivyo waandishi wa habari mnao wajibu mkubwa kutumia
taaluma yenu kuelimisha umma umuhimu wa kulipa kodi, Alisema Bw.
Kayombo.
Kayombo
amesema, TRA kwa niaba ya serikali ya ndiyo chombo chenye mamlaka ya
kukusanya kodi za serikali kutoka kwa watu binafsi, makampuni na taasisi
za umma.
“Huduma
za usafiri, elimu, afya na miundombinu itakuwa bora tu endapo wananchi
watatimiza wajibu wao wa kulipa kodi.” Alisema na kuongeza katika semina
hii waandishi wa habari watapata fursa ya kujifunza mambo mbalimbali
yahusuyo kodi ikiwemo kodi ya majengo kutoka kwa watalamu wa kodi wa
TRA.

Afisa
Mawasiliano Mwandamizi wa TRA, Bi. Rachael Mkundai, (kulia),
akiwakaribisha waandishi wa habari kwenye semina. Kushoto ni Mwenyekiti
wa semina, Bi. Angella Msangi .

Mkutano huo ukiendelea

Waandishi wa habari wakifuatilia hotuba ya ufunguzi .
0 MAONI YAKO:
Post a Comment