
Sambulizi la kihalifu mitandaoni
lililotendeka kupitia utumizi wa vifaa vinavyoaminika kuibwa kutoka
kitengo cha ujasusi nchini Marekani NSA limeathiri mashirika tofauti
duniani.
Kampuni ya kulinda uhalifu wa mitandao Avast, imesema
kuwa imeona kesi 75,000 za programu zinazotumika kufanya uhalifu
mtandaoni inayojulikana kama 'WannaCry' duniani.
Kuna ripoti za maambukizi katika mataifa 99 ikiwemo Urusi nchini China.
Kati ya mashirika yalioathirika zaidi ni shirika la huduma za afya nchini Uingereza na Uskochi.
BBC
inaelewa kwamba takriban mashirika 40 na huduma kadhaa za matibabu
ziliathirika huku operesheni na mikutano ikifutiliwa mbali.
Programu
hiyo ilisambaa kwa kasi siku ya Ijumaa ambapo ilitaka malipo ya dola
300 ili kufungua faili ilizokuwa imeziteka nyara katika kompyuta.
Siku nzima, mataifa ya Ulaya yaliripoti maambukizi hayo.
Idadi
kubwa ya kampuni kubwa ikiwemo Telefonica ,kampuni ya umeme ya
Iberdrola na ile ya Gesi asilia pia ziliathirika huku kukiwa na ripoti
kwamba wafanyikazi katika kampuni hizo waliagizwa kuzima kompyuta zao.
Raia
walipiga picha za kompyuta zilizoathirika katika mtandao wa Twitter
ikiwemo mashine ya kukata tiketi za safari ya reli nchini Ujerumani
pamoja na maabara ya kompyuta nchini Italy.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment