Mzee Yusuph
Aliyekuwa mfalme wa muziki wa miondoko ya pwani 'taarab', Mzee Yusuph
amewataka watu wote waliokuwa na nyimbo zake kwenye simu wafanye hima
kuzifuta kwa madai wakiendelea kuzisikiliza watampatisha dhambi katika
hilo.
Mzee
Yusuph amefunguka hayo ikiwa ni masaa machache yamebakia kwa waumini wa
dini ya kiislamu kuanza ibada yao ya kufunga mwezi mtukufu wa
Ramadhani.
"Mimi nikikubali watu
wacheze nyimbo zangu ina maana nimeruhusu dhambi tena ni bora nirudi
kuimba muziki tena, hivyo watu wote waliokuwa na nyimbo zangu kwenye
simu zao wafute na kuacha kusikiliza ili kuepuka dhambi....Nimetenda
sana makosa tena hadharani na kila mtu anajua lakini kwa sasa ninawaomba
tu mniombee dua ili niendelee kuwa salama japo hali yangu kiuchumi
haiko sawa imebadilika nazidi kupambana ili kipatikane kitu"
alisema Mzee Yusuph
Aidha, Mzee Yusuph amesema kwa sasa
hajihusishi na masuala ya muziki wa kidunia tena bali ataendelea
kuitangaza dini yake pamoja na kuimba nyimbo za kaswida.
Pamoja na hayo, Mzee Yusuph amewasihi
waislamu kumrudia Mungu wao kwa kufanya mambo mema katika kipindi hiki
cha mfungo pamoja na kuwataka akina baba kuacha manyanyaso kwa wake zao
majumbani
0 MAONI YAKO:
Post a Comment