Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Annastazia Wambura
amesema kuwa hana taarifa kuhusu waandishi wa habari kukamatwa na polisi
au viongozi mbalimbali wa Serikali na kuzuiwa kutimiza majukumu yao ya
kazi na kuomba mbunge aliyeuliza swali hilo ampe taarifa ya kina baada
ya kutoka bungeni hapo.
Mhe. Wambura alisema hayo leo bungeni wakati akijibu swali la Mbunge
wa Viti Maalum(Chadema), Devotha Minja aliyeuliza msimamo wa Serikali
kuhusu matukio ya uvamizi kwa waandishi wa habari wakiwa katika
utekelezaji wa majukumu yao ya kazi.
Hata hivyo Mbunge Minja pia alihusisha tukio la jana la waandishi wa
habari wa vituo mbalimbali vya habari Arusha kukamatwa na polisi
wakiunganishwa na Meya wa Arusha, Calist Lazaro na wamiliki wa shule
binafsi, walipokua wakitoa salamu za rambirambi katika Shule ya Lucky
Vincent.
“Anaposema kuna watu wanashindwa kufanya kazi zao. Mimi naamini kama
kweli waandishi wa habari wanafuata maadili na wanatafuta habari
kwaajili ya kujenga na sio kuvuruga nchi siamini kama kuna watu wanaweza
kuja kuwazuia,” alisema Wambura.
“Mimi ndio kwanza nasikia kutoka kwako mheshimiwa Mbunge, naomba
baada ya kutoka hapa tuonane ili unipatie taarifa kwa kina kuhusu hayo
matukio ya kukamatwa waandishi au kuzuiwa kutimiza majukumu yao ya kazi,
Sasa kama kuna hili la wanaozuia noamba Muheshimiwa Devotha Minja aweze
kuniambia ni wapi kwasababu ndio kwanza nasikia hilo. Sera yetu
inaeleza kwamba ni wajibu kwa maafisa wa habari kuwapa ushirikiano
wanahabari kwasababu jukumu lao linatambulika kisheria.”
0 MAONI YAKO:
Post a Comment