Mchezaji wa timu ya taifa ya Ureno na klabu ya Real Madrid, Cristiano Ronaldo usiku wa jana amefanikiwa kuvunja record iliyowekwa miaka 46 iliyopita na mchezaji , Jimmy Greaves , ya Kuongoza kwa jumla ya Ufungaji wa magoli ya Ulaya na kuisadia klabu yake ya Real Madrid kunusa ubingwa wa ligi ya nchini Hispania kwa tofauti ya alama tangu 2012
Ronaldo,mwenye umri wa miaka 31, ameifikisha Madrid kuwa kileleni baada ya kushinda goli lake la 367 katika mabao yake yote ya Ulaya, kwenye ligi kuu tano bora za Ulaya , historia ambayo iliwekwa na Legendari wa Uingereza , mshambuliaji,Greaves mwaka 1971.
Katika mchezo huo ambao Real Madrid ilichomoza na ushindi wa magoli 4 kwa 1 dhidi ya klabu ya Celta Vigo, mchezaji huyo alitupia goli moja kati ya hayo, sasa Madrid inahitaji sare yoyote katika mchezo wake wa mwisho wa ligi wakatapo kutana na klabu ya Malaga jumapili hii , ili kujitangazia Ubingwa wa Ligi.
Katika Mchezo wa hapo Jana Real Madrid imeonekana kuzidiwa licha ya Ushindi walioupata.
‘Sijiskii kama vile tumeshakuwa mabingwa hapana bado
“Tumesalia mchezo mmoja lakini siku ya leo ilikuwa muhimu sana . Tunafahamu ni ni tunahitaji kufanya . Tunahitaji kujiandaa vyema na kujiweka sawa kuanzia leo”.
Goli la 367, la Cristian Ronaldo katika mchezo wao na Celta Vigo uliomalizika kwa matokeo ya 4 kwa 1
“Sihitaji kujiskia kama tayari sisi ni Mabingwa, bado tunahitaji alama zaidi na hicho ndio kitu tunachotaka kufanya”.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment