
Picha ya baadhi ya wasichana wa Chibok waliotekwa nyara muda mfupi mwezi Mei 2014
Ofisi kuu ya Rais wa Nigeria
imethibitisha kuwa wanafunzi 82 wa shule ya wasichana wa Chibok,
waliotekwa nyara na wanamgambo wa kiislamu wa Boko Haram mnamo mwaka wa
2014, wameachiwa huru.
Maafisa wanasema kuwa waliachiwa huru,
kufuatia majadiliano ya muda mrefu na ubadilishanaji washukiwa wa Boko
Haram, waliokuwa wamezuiliwa na wakuu wa nchi hiyo.
Wasichana hao
ni miongoni mwa zaidi ya wanafunzi wanafunzi 270 waliotekwa nyara kutoka
shule ya malazi katika mji wa Chibok ulioko kaskazini mashariki mwa
Nigeria.Wasichana hao wote 82 kwa sasa wanalindwa na jeshi la Nigeria mahali
salama, baada ya kuletwa kwa barabara kutoka maeneo ya ndani kabisa
vijijini, hadi katika kambi ya jeshi ya Banki, karibu na mpaka na
Cameroon, hayo ni kwa mjibu wa mwaandishi habari wa BBC Stephanie
Hegarty kutoka Lagos.

Wasichana 21 walioachiwa huru Oktoba 2016
Mwaandishi wetu anasema kuwa, familia nyingi huko Chibok wamefurahia
taarifa hiyo ya hivi punde lakini wapiganaji hao wa Boko Haram, wangali
wakiwazuilia zaidi ya wanafunzi 100.i sehemu ya maelfu ya watu ambao wametekwa nyara na wanamgambo hao, walioanzisha vuguvugu hilo miaka minane iliyopita.
Utekaji nyara huo ambao ulifahamika baadaye kama "Chibok girls"
ulisababisha kilio kikubwa kote duniani na kampeini za kutaka waachiwe
huru ikatanda kote katika mitandao ya kijamii.
Kabla ya hatua hii ya hivi punde ya kuwaachia wasichana hao, inakisiwa kuwa zaidi ya wasichana 195 wangali hawajulikani waliko.
Idadi ya washukiwa wa Boko Haram ambao wameachiwa huru na utawala wa Nigeria, bado haijajulikana.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment