Afisa
wa Bank ya UBA Tanzania, Bi Mtinta Joseph Ringa pamoja na afisa wa bank
Bw. Sihika Malunguja wakifurahi kumuhudumia mmoja wa wateja
aliyetembelea banda la bank ya UBA Tanzania katika Maonyesho ya 41 ya
kibiashara Tanzania yaliyoanza hivi karibu. Bank ya UBA inawakaribisha
wateja wote kuweza kufika katika banda lao kwaajili ya kujipatia huduma
mbalimbali za kibenki ikiwemo na kufungua akaunti na kujipatia kadi mpya
ya Mastercard ambayo unaweza kuwa nayo bila kuwa na akaunti.
Afisa
wa benki ya UBA Tanzania, Bw Fahimu Zuberi akimpatia maelezo kuhusiana
na kadi mpya za mastercard mmoja wa wateja waliotembelea banda la benki
hiyo lililopo katika banda la Sabasaba kwenye maonyesho ya 41 ya
kibiashara ya kimataifa yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Nyerere
vilivyopo barabara ya Kilwa Jijini Dar Es Salaam
Afisa
wa benki ya UBA Tanzania, Bw Fahimu Zuberi akiendelea kumpatia
maelekezo ya kina kuhusiana na kadi mpya mpya za mastercard ambazo mteja
anaweza kuwa nayo bila kuwa na akaunti ya benki
Wafanyakazi
wa benki ya UBA Tanzania waliopo kwenye banda lao katika maonyesho ya
41 ya kimataifa ya biashara wakiwa katika picha ya pamoja huku
wakifurahia kuwahudumia baadhi ya wateja waliofika katika banda lao huku
wakiwakaribisha wateja kufika katika banda lao na kujipatia huduma
mbalimbali za kibenki.
Picha zote na Josephat Lukaza – Lukaza Blog
0 MAONI YAKO:
Post a Comment