Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Doto James (Kushoto) na Mkurugenzi
Mkazi wa Benki ya Dunia anayehudumia nchi za Tanzania, Somalia, Malawi
na Burundi, Bella Bird, wakitia saini makubaliano ya Benki ya Dunia
kuipatia Tanzania mkopo wenye riba nafuu wa Dola za Marekani milioni 80
kwa ajili ya kutekeleza maboresho ya elimu ya msingi na sekondari
kupitia mpango wa lipa kwa matokeo (elimu bila malipo), Jijini Dar es
Salaam.

na Burundi, Bella Bird, wakibadilishana hati (mkataba) ya mkopo wenye
riba nafuu wa Dola za Marekani milioni 80 kwa ajili ya kutekeleza
maboresho ya elimu ya msingi na sekondari kupitia mpango wa lipa kwa
matokeo (elimu bila malipo), jijini Dar es Salaam.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw, Doto James akizungumza na
waandishi wa habari (hawapo pichani) baada ya kutia saini makubaliano na
Benki ya Dunia ya kuipatia Tanzania mkopo wenye riba nafuu wa Dola za
Marekani milioni 80 kwa ajili ya kutekeleza maboresho ya elimu ya msingi
na sekondari kupitia mpango wa lipa kwa matokeo (elimu bila malipo), Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi
Mkazi wa Benki ya Dunia anayehudumia nchi za Tanzania, Somalia, Malawi
na Burundi, Bi. Bella Bird, akisisitiza jambo mbele ya waandishi wa
habari (hawapo pichani) baada ya kusaini makubaliano ya Benki yake ya
kuipatia Tanzania mkopo wenye riba nafuu wa Dola za Marekani milioni 80
kwa ajili ya kutekeleza maboresho ya elimu ya msingi na sekondari
kupitia mpango wa lipa kwa matokeo (elimu bila malipo), Jijini Dar es
Salaam. (Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-WFM)
BENKI
ya Dunia imeipatia Tanzania mkopo wenye masharti nafuu wa Dola za
Marekani milioni 80 kwa ajili ya kusaidia mpango wa Serikali wa miaka 11
wa Elimu bila malipo kuanzia elimu ya msingi hadi sekondari nchini.
Kiasi
hicho cha fedha ni nyongeza ya Dola milioni 122 zilizotolewa na Benki
hiyo katika awamu ya kwanza ya utekelezaji wa maboresho ya elimu kupitia
Mpango wa Tekeleza kwa Matokeo Makubwa sasa-BRN, uliolenga kuondoa
changamoto za elimu nchini.
Mkurugenzi
Mkazi wa Benki ya Dunia anayehudumia nchi za Tanzania, Somalia, Malawi
na Burundi, Bella Bird amesema wakati wa utiaji saini mkataba wa
nyongeza ya fedha hizo kati yake na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na
Mipango Bw. Doto James, kuwa nyongeza ya Dola milioni 80 imetokana na
Benki hiyo kuridhishwa na namna Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa
na Dokt. John Pombe Magufuli, ilivyosimamia kikamilifu mpango huo wa
utoaji elimu bure na kuwanufaisha wanafunzi wengi wakiwemo wanaotoka
katika familia masikini.
Amesema
kuwa uamuzi huo umesababisha ongezeko kubwa la wanafunzi wanaojiunga na
elimu ya msingi, kuongezeka kwa ufaulu, wanafunzi kujua maarifa ya
hesabu, kusoma na kuandika, utoaji wa ruzuku ya elimu kwa wakati, hatua
ambayo pia imesababisha kuwepo kwa changamoto za ukosefu wa miundombinu
ya shule, changamoto ambazo anaamini zinapungua kupitia mkopo huo wenye
masharti nafuu.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Doto James ameishukuru Benki ya
Dunia kwa kutoa fedha hizo ambazo amesema zitasaidia kwa kiasi kikubwa
mipango ya Serikali ya kuboresha elimu nchini na kuondoa changamoto
zinazoukabili mpango huo likiwemo ongezeko hilo kubwa la wanafunzi.
Bw.
James ameeleza kuwa fedha hizo zitasaidia ujenzi wa miundombinu ya
madarasa, ubora wa eimu, ukaguzi wa shule, upelekaji wa walimu, na
kuwasaidia wanafunzi wenye mahitaji maalumu ili waweze kupata haki hiyo
ya msingi ya elimu.
Kwa
upande wake Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia
Prof. Simon Msanjila, amesema kuwa katika awamu ya kwanza ya utekelezaji
wa mradi wa elimu wa lipa kulingana na matokeo upitia mkopo wenye
masharti nafuu wa Dola za Marekani milioni 122 zimetumika kujenga
madarasa 1,400, matundu 3,390 ya vyoo, mabweni 261, majengo ya utawala
9, mabwalo ya chakula 9 nyumba za walimu 11, uchimaji wa visima vya maji
katika shule nne na kukarabati vyuo vya ualimu.
Amesema
kuwa mkopo mpya wa dola za Marekani milioni 80 uliotolewa na Benki ya
Dunia hata kabla ya awamu ya kwanza ya mradi huo kumalizika hapo
mwakani, umeonesha nia ya dhati ya Benki ya Dunia kusaidia maendeleo ya
elimu nchini.
Benny Mwaipaja, WFM-Dar es Salaam
0 MAONI YAKO:
Post a Comment