Mbunge wa Mikumi na rapa mkongwe nchini Tanzania, Mh. Joseph Haule.
Mbunge wa Mikumi na rapa mkongwe nchini Tanzania, Mh. Joseph Haule
maarufu kama Prof. Jay amefunguka kwa kudai harusi yake imekuwa yenye
baraka kutoka kwa Mungu maana ameweza kuwakutanisha viongozi wa kisiasa
kwa pamoja bila ya kujali itikadi zao.
Haule
amebainisha hayo kupitia kipindi cha 'Friday Night Live' kinachorushwa
na EATV baada ya kuulizwa ni jambo ni gani hasa liliweza kumvutia katika
harusi yake.
"Kikubwa kabisa
ninachomshukuru Mungu mbele za haki kabisa ni kwamba nimejitahidi
kuunganisha hata siasa zetu za Tanzania ambazo zipo kwa kuwaunganisha
viongozi wetu, watu wa vyama vyote walikuwa pale, watu wa dini zote
walikuwa pale, kile ni kitu kikubwa kiukweli", amesema Haule.
Pamoja na hayo, Haule amedai siku mbili
kabla ya harusi yake, alikuwa ni mtu mwenye wasiwasi katika nafsi yake
kwamba isije ikatokea akamkana mkewe mbele ya Padri wakati wa
kufungishwa ndoa.
"Nilikuwa na hofu kubwa na
presha ilikuwa inapanda na ndiyo maana hata wanangu wengine sijaongea
nao kwa muda mrefu hata simu yenyewe nilikuwa ninaiyogopa. Nikawa nasema
isije siku Padri ananiuliza pale nikasema simtaki kabisa huyu mtu au
yeye akasema hapana, kuna vitu vingi tumeshaona huko vikitokea kwa watu
waliyopita kwa hiyo kusikia kile kitu kimeenda vizuri ni kitu cha
kumshukuru sana Mungu ila hofu ilikuwa kubwa sana", amesisitiza Haule.
Maharusi wakipewa mkono wa dua mara wakati wakikamilisha Ibada ya Ndoa.
Katika hatua nyingine, Haule amesema
mwanaye Lisa ameamuahidi anaenda kufaulu mtihani wake wa kuhitimu darasa
la saba kwa kuwa jambo ambalo alilokuwa analisubiri kuliona kwa muda
mrefu limetimia kwa wazazi wake.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment