Waziri
Mkuu alisema hayo jana wakati alipotembelea kiwanda cha nyuzi cha
Namera kilichoko Gongo la Mboto na kiwanda cha nguo cha Nida kilichopo
Ubungo Dar es Salaam ambapo alidai viwanda vya kutengeneza nguo nchini
ni ushahidi tosha kwamba nchi iko njiani kuondokana na matumizi ya nguo
za mitumba kwa kuwa nguo nyingi zitakuwa zinatengenezwa nchini, hivyo
kupatikana kwa bei nafuu.
Mbali na hilo Waziri Mkuu aliwapa matumaini wakulima wa pamba na kusema hawana sababu ya kwenda kuuza nje ya nchi na badala yake wauze pamba hiyo katika viwanda vya ndani ili vizalishe nguo za kutosha zitakazouzwa nchini kwa gharama nafuu.
“Pamba yote inaweza kuchakatwa nchini, hivyo hakuna haja ya kuiuza nje ya nchi. Natoa wito kwa wakulima wetu wa pamba walime mazao ya kutosha kwa sababu soko la uhakika lipo na hii ndio safari ya mwisho ya mitumba Tanzania" alisema Waziri Mkuu
Mbali na hilo Waziri Mkuu alitoa wito kwa wamiliki wa viwanda vyote nchini kuhakikisha wanatoa kipaumbele cha ajira kwa wananchi waishio katika maeneo ya karibu na viwanda hivyo sambamba na kulipa kodi kwa wakati na kwa viwango sahihi.

0 MAONI YAKO:
Post a Comment