Msemaji wa Simba, Haji Manara ameamua kufanya "uchale" baada ya kuiwakilisha Yanga wakati wa hafla fupi ya ukabizishwaji vifaa iliyofanywa na wadhamini wa Ligi Kuu Bara, Vodacom.
Manara alikwenda moja kwa moja jukwaani wakati vijana waliokuwa wakiiwakilisha Yanga kupanda jukwaani kutambulisha jezi hizo.
Kwa
kuwa hakukuwa na mwakilishi wa Yanga, Manara alipanda jukwaani na
kusema anawawakilisha akifanya utani ingawa baadhi walimpongeza na
kusema aliiwakilisha timu ya baba yake, Sunday Manara, naye akasema
hawezi kuwa Yanga hadi anakufa.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment