August 12, 2017

  Image result for Wallace Karia 
 
Na Mwandishi Wetu, DODOMA
WALLACE KARIA ndiye Rais mpya wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), baada ya kuibuka kidedea katika uchaguzi uliofanyika leo kwenye ukumbi wa mikutano wa jengo la St. Gasper mjini Dodoma.
Karia amewashinda mchezaji wa zamani wa timu ya taifa, Ally Mayay, Katibu wa zamani wa shirikisho hilo, Frederick Mwakalebela, Mwenyekiti wa zamani wa klabu ya Yanga, Wakili Imani Madega, Mwandishi wa Habari za Michezo wa zamani, Shija Richard na Katibu wa klabu ya Mbeya City, Emmanuel Kimbe.
Michael Richard Wambura ameshinda nafasi ya Umakamu wa Rais akiwaangusha Mwenyekiti wa FA ya Dodoma, Mulamu Nghambi, mchezaji wa zamani wa timu ya taifa, Mtemi Ramadhani, Robert Selasela na Stephen Mwakibolwa. Baada ya matokeo hayo, washindi wote wa waliapishwa kwa agizo la Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe
Ikumbukwe aliyekuwa Rais wa TFF, Jamal Malinzi ameshindwa kurudi kutetea nafasi yake baada ya kuweka rumande tangu Juni 29, mwaka huu kwa pamoja na Katibu weke, Selestine Mwesigwa na Isinde Isawafo Mwanga kwa tuhuma za ubadhirifu.
Watatu hao walipelekwa rumande Juni 29 baada ya kusomewa mashitaka 28 ya kughushi na kutakatisha fedha kupitia akaunti ya TFF iliyopo katika banki ya Stanbic, Dar es Salaam.
Katika mashitaka hayo, 25 yanakwenda moja kwa moja kwa Rais wa shirikisho hilo, Malinzi akidaiwa kughushi michakato mbalimbali ya kifedha, huku matatu yakiwahusu wote na Katibu wake na Mhasibu wake Nsiande Isawafo Mwanga.
Malinzi aliingia madarakani TFF Oktoba mwaka 2013 baada ya kupata kura 72 kati ya 126 zilizopigwa akimshinda aliyekuwa mpinzani wake wa karibu, Athumani Nyamlani, lakini baada ya kesi hiyo kuanza kuunguurma na kuwekwa rumande, Kamati ya Utendaji ya TFF ilikutana na kumteua Makamu wake, Wallace Karia kukaimu Urais wa shirikisho hilo.

Related Posts:

  • JINSI KURA ZA BALLON D' OR NA LIST YA WASHINDI HII HAPA Dakika chache zilizopita zimefanyika tuzo za Ballon d’Or ambapo wachezaji wa mwaka uliopita walikuwa wakitunukiwa na shirikisho la soka ulimwenguni, FIFA. Mwanasoka bora wa msimu uliopita mreno Cristiano Ronaldo a… Read More
  • GAVAO LODGE INATOA HUDUMA MASAA 24   GAVA LODGE INAKUTAHARIFU WEWE MTEJA WAKE KUWA SASA IMEFUNGULIWA RASMI NA INATOA HUDUMA MASA 24. GAVAO LODGE IPO KIHONDA YOUTH MISSION MKOANI MOROGORO, MITA CHACHE KUTOKA BARABARA YA DODOMA. GAVAO LODGE INAKUPA HUDUMA … Read More
  • MKE WA AMINI AJIFUNGUAKWA OPARESHENI,MTOTO BAHATI MBAYA   Mke wa msanii  wa muziki  Amini, Farida akiwa na mimba.   Msanii wa Bongo Flava, Amini. Mke wa msanii  wa muziki  Amini, Farida jana jioni alijifungua kwa operesheni lakini kwa bahati mt… Read More
  • NEW AUDIO/ MADEE- VUVULA Rais wa Manzese Hamad Ally almaarufuMADEE toka kundi la Tip Top Connection, hapa anakupa nafasi ya kusikiliza wimbo wake mpya kabisa unaoitwa VUVULA uliofanywa na producer DJMAPHORISA … Read More
  • GAVAO LODGE INATOA HUDUMA MASAA 24   GAVA LODGE INAKUTAHARIFU WEWE MTEJA WAKE KUWA SASA IMEFUNGULIWA RASMI NA INATOA HUDUMA MASA 24. GAVAO LODGE IPO KIHONDA YOUTH MISSION MKOANI MOROGORO, MITA CHACHE KUTOKA BARABARA YA DODOMA. GAVAO LODGE INAKUPA HUD… Read More

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE