September 30, 2017

Suala la Neymar bado ni bichi na inaonekana wazi kwamba Barcelona bado hawajaridhika na mchakato huo jinsi ulivyokwenda pamoja na ukweli kwamba tayari Neymar ameanza kuvaa jezi ya PSG.
Barcelona wameamua kurudi tena mahakamani kuishitaki PSG pamoja na wawakilishi wa Neymar kuhusu kiasi cha pesa ya ziada ambayo Barcelona waliitoa kwa wawakilishi wa Neymar wakati akienda PSG baada ya mchakato wa usajili kukamilika.
Gazeti moja maarufu la michezo nchini Hispania linasema kesi ya kwanza kati ya Barcelona na PSG ilimalizika na kila kitu kikaenda sawa lakini sasa Barcelona wameibuka upya na madai mengine kuhusu pesa hizo zaidi ya euro 26m.
Barcelona wanaamini kuna rushwa ilitembea kwenye upande mmoja wa usajili huku baba mzazi wa Neymar naye akihusishwa katika kesi hiyo ambapo Barcelona wanahitaji kiasi cha euro 8.6m kama fidia.
Baba mzazi wa Neymar na upande wa wawakilishi wa Neymar wanadaiwa walipokea zaidi ya euro 26m wakati wa mchakato wa usajili huo kitu ambacho kimewafanya Barcelona kuhisi kuna rushwa ilitendeka.
Tayari kesi hii imepelekwa mbele ya mahakama ya FIFA na pande zote tatu yaani Barcelona, baba mzazi wa Neymar ambaye ndio muwakilishi wake na PSG watakutana siku ya Jumanne kuanza kujadili kesi hii

Related Posts:

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE