
Mbunge wa Iringa Mjini Peter Msigwa (Chadema)
amekamatwa na polisi leo Jumapili jioni baada ya kushushwa jukwaani
kwenye mkutano wa hadhara katika Kata ya Mlandege mkoani Iringa.
Mwenyekiti
wa Baraza la Vijana wa Chadema Iringa Mjini (Bavicha), Leonce Marto
amesema kuwa mbunge huyo alikamatwa saa 11:24 jioni na Mkuu
wa Upelelezi wa Mkoa (RCO) aliyekuwa ameambatana na polisi wengine
kisha wakampeleka ofisi za mkoa za jeshi hilo.
“Kutoka
Mlandege mpaka ofisini kwa kamanda wa mkoa amebadilishwa kwenye magari
matatu. Tunahisi atakuwa anasafirishwa ingawa bado anahojiwa. Yupo
ndani, sisi tunaendelea kumsubiri nje,” amesema Marto.
Mwenyekiti
huyo alizungumza na Mwananchi kupitia simu ya mbunge huyo na kubainisha
kwamba mpaka wakati huo (saa 12:30 jioni) jeshi hilo halikubainisha
sababu za kumshikilia Msigwa.
“Alikuwa na kibali cha
kufanya mkutano katika kata tatu kuanzia leo Jumapili mpaka Jumanne.
Alianza kuzungumza saa tisa alasiri ilipofika saa 11:24 jioni, RCO akiwa
na polisi wengi wakamshusha jukwaani na kuondoka naye,” alisema Marto
bila kufafanua sababu za kukamatwa.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment