Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Dodoma, Gilles Muroto amemtaka dereva wa
Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Antiphas Lissu, ajitokeze ili aweze
kutoa maelezo yake kuhusiana na tukio la kupigwa risasikwa bosi wake.
Kamanda
huyo amesema kwamba sababu ya kumtafuta dereva huyo aliyemtaja kwa jina
moja la Adam ni kwa sababu alikuwa pamoja na majeruhi wakati tukio hilo
linatokea lakini tangu kutokwea kwa tukio hilo dereva huyo hajaonekana.
"Tangu kutokea kwa tukio
dereva hakuonekana. Lakini kupitia gazeti tumeona ameanza kufanya
mahojiano jana. Sasa amewezaje kufika Dar es salaam na Dodoma asifike.
Sababu za kutoonekana hazifahamiki. Dereva huyo ni mtu muhimu kwetu
katika kutoa ushahidi. Natoa 'notice' afike ofisi ya Mkurugenzi wa
makosa ya jinai Dar au ofisi ya Mkuu wa makosa ya jinai Dodoma atupe
taarifa zinazohusiana na tukio hili. Tunaamini anazo siri za tukio hilo.
Kamanda Muroto ameongeza kuwa "Sheria yetu inasema mtu aliye na taarifa akashindwa kuzitoa kwa jeshi la polisi atakuwa amefanya mako. Na kwa nini asitoe.
Pia Kamanda huyo alimtaka Katibu Mkuu wa
Chadema Dkt. Vicent Mashinji kufika kwa RCO mjini Dar es Salaam ama
Dodoma kutokana kauli yake kuwa katika uchunguzi wao wamewabaini
wahusika.
Amemtaka kutoa taarifa kwa jeshi la
polisi kwa sababu kuonekana kwenye magazeti haitoshi bali kushirikiana
kama mwananchi ndiyo njia sahihi ya kuwabaini wahalifu.
Pamoja na hayo Kamanda Muroto ameongeza kuwa
"Tukio
hili lisichukuliwe kama mtaji wa kisiasa. Nimesikia chama fulani
kinahamasisha watu kutoa damu. Nawaomba watulie watuachie polisi nafasi
ya kufanya kazi yetu. Matokeo mengi yameshatokea ikiwepo mauaji ya
Kibiti, Mauaji ya Askari wetu lakini jeshi la polisi lilifanya uchunguzi
na kubaini".
0 MAONI YAKO:
Post a Comment