Mkongwe wa muziki Bongo, Jay Moe amedai kuwa hawezi kununua views katika mtandao wa YouTube kwani kufanya hivyo ni kujidanganya.
Rapper huyo ambaye kwa sasa anafanya vizuri na ngoma yake mpya ‘Me and You’ amefunguka hayo kupitia The Playlist ya Times Fm na kueleza alishawahi kushawishiwa kufanya hivyo lakini hakukubali.
Rapper huyo ambaye kwa sasa anafanya vizuri na ngoma yake mpya ‘Me and You’ amefunguka hayo kupitia The Playlist ya Times Fm na kueleza alishawahi kushawishiwa kufanya hivyo lakini hakukubali.
“No! no! ningekuwa tayari kufanya hivyo (ningefanya), mimi
nimeshawishiwa na watu tangia Nisaidie kushare na hao watu hadi leo
wananilaumu siunaona hadi leo hatujafika views milioni moja. Wananiambia
we can do numbers kwenye mazingira haya na haya lakini mimi mwenyewe
inaweza isiwe actual namba zangu, kwamba namba zangu halali ni hizi,”
amesema Jay Moe.
Katika hatua nyingine msanii huyo amesema mitandao ya kijamii
imesaidia sana wasanii wa sasa kukua na kujulikana, hata hivyo ameonya
kuwa kama isingekuwepo kuna wasanii wasingesisikika na si kwa Tanzania
pekee bali hata dunia nzima.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment