MFANYABIASHARA Yusuf Manji ameieleza Mahakama ya Hakimu
Mkazi Kisutu leo September 9, 2017 kuwa yeye bado ni Diwani wa Kata ya
Mbagala Kuu na kudai kuwa hatambui kuvuliwa udiwani kama ilivyotangazwa
na Mstahiki Meya wa Temeke, Abdallah Chaulembo September 6, 2017.
Amedai kama ni kweli amevuliwa Udiwani hatambui, kwani ana miezi 2 yupo gerezani na serikali inatambua kwamba yeye ni Diwani.
“Vikao vya awali vya udiwani wa Halmashauri ya Temeke nilikuwa nahudhuria kwa kuwa naheshimu Mahakama na kwa uzito wa hii kesi sikutaka kupeleka hata maombi ya dhamana Mahakamani,Mahakama imuagizie DPP na aiambie Halmashauri ya Temeke kwamba wamenikamata na ndio sababu ya kutohudhuria vikao,Kama wanataka nihudhurie DPP aombe remove order nitolewe gerezani ili niende kwenye vikao.”
Pia Manji amedai kuwa kama hilo haliwezekani, basi wamuandikie barua itakayoonyesha agenda ya vikao vyote na yeye atazijibu kwa njia ya barua pia
“Ninachotambua mimi ni Diwani wa Mbagala Kuu na kama nimevuliwa au sijavuliwa udiwani sitambui. Tayari nimetumia fedha zangu mwenyewe zaidi ya Tsh. Milioni 70 sio za Halmashauri kwa ajili maendeleo ya wananchi wake.”
Aidha, amedai kuwa hiyo kesi ni nzito na DPP hapaswi kuangalia upande wake wa kesi tu, kwani yeye amechaguliwa na wananchi na anawasaidia.
Awali kabla ya kuelezwa hayo, Wakili wa utetezi Seni Malimi alidai
kuwa wanatarajia kuwasilisha maombi ambayo ni ya siri katika tarehe
ijayo,Baada ya kuelezwa hayo Hakimu Huruma Shaidi akautaka upande wa
mashtaka kuhakikisha wanalifanyia kazi suala hilo ambapo kesi
imeahirishwa hadi September 18, 2017.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment