Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Nyakoro Sirro amefunguka na
kusema kuwa jeshi la polisi linatambua makosa ya kimtandao yanayofanywa
na mwanadada Mange Kimambi na kusema kuwa jeshi la polisi
linashughulikia suala hilo.
IGP
Sirro amesema hayo leo alipokuwa mjini Iringa kwenye ziara ambapo
amesema kuwa jeshi la polisi linatambua uvunjifu wa sheria ya makosa ya
kimtandao yanayofanywa na mwadada huyo maarufu mitandaoni ambaye amekuwa
mkosoaji wa mambo mbalimbali na kutoa machapisho ambayo serikali inaona
ni ya matusi na kashfa kwa serikali na viongozi wake.
Aidha IGP Sirro amesema kuwa kwa sasa hawawezi kuweka wazi ni hatua
gani zinachukuliwa dhidi ya mwanadada huyo ambaye kwa sasa anaishi
nchini Marekani
Mbali na hilo IGP Sirro amesema jeshi hilo halitawavumilia maafisa
wa polisi na askari wanaowasaidia watu wanaofanya unyanyasaji kwa watoto
kwa kuwafanyia vitendo vya ubakaji na ulawiti ili kukwepa mkono wa
sheria huku akiwataka wananchi wanaohisi kutotendewa haki katika
kushughulikia makosa ya aina hiyo kupeleke malalamiko kwa wakuu wa mikoa
na viongozi wengine





0 MAONI YAKO:
Post a Comment