Katibu mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Prof. Kitila Mkumbo,
amejiuzulu uanachama wa ACT-Wazalendo baada ya kudai anapata ugumu
kutumikia vitu viwili kwa pamoja.
Katika
Barua ambayo imetolewa leo na kusambaa mitandaoni ambayo Kitila Mkumbo
amekiri ni ya kwake, amesema kwamba ameona kuna mgongano wa kimaslahi
anaoupata kwa kutumikia Ukatibu Mkuu wa wizara, huku akiwa amevaa
uanachama cha ACT- Wazalendo.
"Katika maelezo niliyoyaandika hapo juu na ili kuepuka mgongano wa
wazi wa maslahi, nimeamua kung'atuka uanachama wangu wa ACT- Wazalendo,
kuanzia terehe iliyoonyeshwa chini ya barua hii", ilisomeka sehemu ya
barua hiyo.
Kitila Mkumbo amesema uamuzi zaidi anauachia uongozi wa chama cha
ACT- Wazalendo, na huku akiwashukuru kwa ushirikiano kwa muda wote ambao
walikuwa kwenye chama.
Soma barua yote hapo chini, na sauti akisikika akikiri kuwa barua hiyo ni yake kweli.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment