Karibu kwa taarifa za moja kwa moja. Kituo cha matangazo cha serikali kinasema kuwa Rais Robert Mugabe atahutubia taifa muda mfupi unaokuja.
Mugabe: Yaliyotokea yamedhihirisha msingi wa amani
Amesema yaliyotokea wiki iliyopiya yamedhihirisha msingi wa amani na demokrasia nchini Zimbabwe.
Aidha, kujitolea kwa watu wa Zimbabwe kutatua mizozo kwa amani - jambo ambalo ni nadra sana katika nchi nyingine.
"Ni rasilimali muhimu sisi hutumia nyakati za dhiki," amesema
Nguzo za serikali zilisalia kuwa imara
Mugabe amesema hata wakati wa mzozo wa sasa, mfumo wa mamlaka uliendelea kuheshimiwa. Amesema hilo lilidhihirika pia hata katika mkutano wa leo.
'Mizozo sasa itakoma, na raia watafaidi'
Amesema mizozo na mivutano ambayo ilikuwa imekwamisha shughuli nyingi nchini humo sasa itakoma.
Serikali itajizatiti kuimarisha hali ya wananchi kiuchumi na kimaendeleo.
Amesema serikali itazindua mpango mkubwa wa ujasiamali wa kuwafaa hata raia maeneo ya mashinani.
waliopigania uhuru watatekeleza mchango muhimu
Mugabe amesema kunao waliopigania uhuru ambao bado wapo na kwamba ni lazima waendelee kutekeleza mchango muhimu katika uongozi wa taifa.
Amesema ni muhimu kuwalipa.
Uongozi wa 'kiimla' lazima ukome
Enzi ya kuwalaumu baadhi ya watu na maamuzi ya kiimla sharti ikome.
"Lazima tutambue kwamba Zanu-PF ni chama cha utamaduni na kimeongoza na utamaduni wa muda mrefu wa maadili ambao lazima uendelee," amesema.
"Masuala ya mizozo ya marika ni lazima itatuliwe kwa kuoanisha kwa njia nzuri wale wazee na wale wa vizazi vipya kwa kufuata mfumo unaoeleweka wa kutoa amri na urithi."
Amesema hayo yatajadiliwa katika mkutano mkuu ujao wa chama kuondoa shaka na mambo ambayo yameathiri chama hicho.
"Mkutano utafanyika wiki chache zijazo. Nitaongoza shughuli zake," amesema.
Hatuwezi kuongoza na machungu na kulipiza kisasi
Bw Mugabe amesema: "Hatuwezi kuongozwa na machungu au ulipizaji kisasi, hayawezi kutufanya wanachama wema au raia wema.
"Sera yetu ya maridhiano tuliyotangaza miaka ya 1980 ambayo tulitumia hata kwa waliotudhalilisha kwa miaka mingi na tuliopigana haiwezi kosa kutumiwa kwa wenzetu - ndani ya chama na hata nje.
"Lazima tujifunze kusameheana na kutatua mizozo yetu, halisi na ya kudhaniwa. Kwa urafiki.
"Tusonge mbele, tukijikumbusha kuhusu kauli mbiu yetu ya wakati wa vita."
Mugabe amemalizia hotuba yake kwa shukrani kwa lugha kadha, miongoni mwake amesema 'Asante sana'.

0 MAONI YAKO:
Post a Comment