Baada ya kuvuliwa nafasi ya kiongozi wa juu wa Chama cha Zanu- PF
Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe amepewa masaa tu na Chama hicho
kujiuzulu mwenyewe kwenye nafasi ya Urais wa nchi hiyo bila kutumia
nguvu.
Chama tawala nchini humo leo baada ya kutangaza kuwa kimemvua uongozi
Rais huyo mkongwe zaidi barani Afrika, Robert Mugabe, kimemwambia hadi
kesho saa 6 mchana awe tayari ametangaza kujiuzulu nafasi ya Urais huku
kikimuonya kuwa endapo atakaidi nguvu ya ziada itatumika kumng’oa
madarakani.
“Rais wetu wa zamani, Robert Mugabe amepewa muda hadi kesho
jumatatu saa 6 mchana awe ameshatangaza kujiuzulu nafasi ya Urais wa
Zimbabwe la sivyo nguvu itatumika kumng’oa madarakani.”Imeeleza taarifa kutoka kwenye chama cha Zanu-PF iliyochapishwa kwenye ukurasa wao rasmi wa Twitter.




0 MAONI YAKO:
Post a Comment